ROHO MTAKATIFU NA VIPAWA |BY PRINCE BEWISA - Fahamu zaidi Staili za Maisha na Saikolojia. Bewisa App | ™ - Efe. 5:15-17
SOMA HIZI PIA:
Loading...

ROHO MTAKATIFU NA VIPAWA



UNAWEZA KUPATA STORI ZETU MOJA KWA MOJA KWA KUBONYEZA 'LIKE' HAPA



« Piga 0652262137 kuweka tangazo lako hapa - Push kwa Buku tu »


1Kor 12:7-11

"Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja;  na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine fasiri za lugha;  lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye."

1. Mungu ameweka karama tofauti tofauti kwa kila mtu kwa njia ya Roho Mtakatifu. Ndio maana watu hatufanani, wewe na mimi, wewe na mke au mume wako, wewe na watoto wako au baba au mama yako, wewe na rafiki zako tupo tofauti sana kutokana na uwekezaji wa karama ambazo Mungu amefanya  ndani yetu kupitia Roho Mtakatifu. 

2. Kusudi la kufanya hizi tofauti ni ili kufaidiana. Kwa hiyo kuna namna Mimi na wewe na yule tunahitajiana kwa sababu ya tofauti tulizonazo. Kuna huduma ambayo Mimi sina nitaipata kwako, kuna ambayo wewe huna utaipata kwangu kwa msaada wa Roho Mtakatifu na Jambo la 3 ni hili:

3. Roho mtakatifu amemgawia karama kila mtu Kama apendavyo yeye. Kwa hiyo kila mtu anayo karama. Hata hivyo mazingira yako ya ibada na kumtafuta Mungu ndiyo yatakayokusaidia kuifunua hiyo karama ili iwe msaada kwa watu wengine.

Kumbuka: Roho Mtakatifu akipewa nafasi na wewe kufanya Kama apendavyo yeye ndani yako kila alichoweka ndani yako hudhihirika katika yeye. Mambo matatu ninakuombea. Ijue karama yako, tengeneza mazingira yako ya kumwabudu Mungu na tatu Roho Mtakatifu atumie karama yako Kama apendavyo yeye. Ubarikiwe. 

Ili kupata Makala zaidi na kwa njia rahisi, Install App yetu kwenye PlayStore. Tafuta BEWIS APA, au BONYEZA HAPA



TUAMBIE UNA MAONI GANI JUU YA HILI?

Facebook Plugin by princebewisa

Chapisha Maoni

Enenda kwa hekima, ukijua ni yapi yaliyo mapenzi ya Mungu huku ukiukomboa wakati. Install Bewisa App kwenye PlayStore kwa maarifa zaidi.
- EV. BENSON W. MMARI, +255 768 111 279

CodeNirvana
© Copyright Bewisa App | ™ - Efe. 5:15-17 | Modified By PB Web and Graphics
Back To Top