MAISHA MAPYA NDANI YA KRISTO |BY PRINCE BEWISA - Fahamu zaidi Staili za Maisha na Saikolojia. Bewisa App | ™ - Efe. 5:15-17
SOMA HIZI PIA:
Loading...

MAISHA MAPYA NDANI YA KRISTO



UNAWEZA KUPATA STORI ZETU MOJA KWA MOJA KWA KUBONYEZA 'LIKE' HAPA



« Piga 0652262137 kuweka tangazo lako hapa - Push kwa Buku tu »

ISAYA 61:10-11

Maisha ni kinyume cha kifo, yaani ukiishi hai ni maisha. Hii huambatana na kukuwa, kustawi na kuzalisha (Mwa. 1:27-28)

Hitimisho la maisha ya mtu ni kifo kimwili; na kiroho ni maisha mengine ya uzima usiokoma. Yaani, mwisho wa maisha ya kimwili ni mwanzo wa maisha mengine kiroho pasipo mwili. 

Maisha ya sasa anayoishi mtu yamebeba hatma (destiny) na kila mmoja anahitajika kuacha alama duniani baada ya kufikia hatma yake; na baada ya hapo uzima wa milele. 

Katika kufikia hatma, mtu hupitia michakato na changamoto mbalimbali zinazomfanya aimarike ama adumae zaidi. Hapo anakuwa na vipindi vya zamani na vya sasa, na vyote vinaamua hatma yake. 

Vipindi vilivyopita vina nafasi ndogo ya kuamua vipindi vijavyo. Nafasi hiyo ndogo ni ile ya kurekebisha makosa tu na kutazama hatma yako katika maisha ya kesho. Havipaswi kutafakariwa sana maana muda ukipita hauwezi kurudishwa. Hapo tunaita maisha yaliyopita ni maisha ya zamani.

Kubadilika kutoka mtazamo wa zamani (mindset) hapo tunaita ni Maisha mapya. Na haya maisha mapya ni mwenendo mpya katika mfululizo wa kuishi kwa mtu.

Mtu hawezi kujibadili, ni mpaka kiwepo kitu kingine kitakachoingilia nafsi yake ili kuzaa mabadiliko. Na ukuu wa mabadiliko hayo utaamuliwa na vitu viwili (Isa. 61:1-11)

  i. Nguvu ya kilichoingilia nafsi

 ii. Namna mtu alivyokipokea

Isaya anaonesha katika 61:10-11 juu ya maisha mapya atakayoyapata mtu baada ya kufutika kwa maisha ya zamani yaliyobeba kinyume cha 61:1-9 lakini chanzo cha hayo maisha ni Roho wa Bwana. Hii inaonesha nguvu ya mabadiliko kwa maisha ya mtu hapo ni Roho wa Mungu ambayo iliingilia fikra za mtu na kuzaa badiliko la maisha na mtazamo ulioleta furaha zaidi. 

Nguvu ya Roho ilitenda kazi na kuleta badiliko. Lakini ili izae zaidi inahitaji mtu anayempokea huyo mtu amwaminj na kumpokea ili huyo Roho apate nafasi ya kushusha mizizi na kuzalisha matunda kwa mhusika. (Yn. 1:12; Mdo. 2:38; Gal. 5:22)

Tunahitiaji kumpokea Yesu Kristo ili abadili hali zetu kila wakati. Ya kale yatapita nayo yatakuwa mapya anaahidi kuwa tukishinda atatuvika taji, hataki tutafakari ya zamani, anaahidi kuchipua kwa chipukizi jipya tukiamini. 

HITIMISHO:

Lakini mwendo wenu na uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, ili, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili; mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia habari zake, iliyohubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paulo nalikuwa mhudumu wake. [Fil. 1:27; Kol. 1:23]

Ili kupata Makala zaidi na kwa njia rahisi, Install App yetu kwenye PlayStore. Tafuta BEWIS APA, au BONYEZA HAPA



TUAMBIE UNA MAONI GANI JUU YA HILI?

Facebook Plugin by princebewisa

Chapisha Maoni

Enenda kwa hekima, ukijua ni yapi yaliyo mapenzi ya Mungu huku ukiukomboa wakati. Install Bewisa App kwenye PlayStore kwa maarifa zaidi.
- EV. BENSON W. MMARI, +255 768 111 279

CodeNirvana
© Copyright Bewisa App | ™ - Efe. 5:15-17 | Modified By PB Web and Graphics
Back To Top