KIKOMBE CHA CHUPA YA CHAI NA MAISHA YAKO |BY PRINCE BEWISA - Fahamu zaidi Staili za Maisha na Saikolojia. Bewisa App | ™ - Efe. 5:15-17
SOMA HIZI PIA:
Loading...

KIKOMBE CHA CHUPA YA CHAI NA MAISHA YAKO



UNAWEZA KUPATA STORI ZETU MOJA KWA MOJA KWA KUBONYEZA 'LIKE' HAPA



« Piga 0652262137 kuweka tangazo lako hapa - Push kwa Buku tu »

 


Mara kadhaa kwenye familia zetu kikombe cha chupa ya chai kimekuwa kikiorodheshwa kwenye idadi ya vikombe vya plastiki alivyonavyo mtu. Lakini mimi napinga hili.

Kikombe cha chupa ya chai si kikombe ila ni sehemu ya mfuniko wa chupa ya chai. Unawezaje kutumia mfuniko na wakati kuna vikombe? Huna tofauti na mtu anayekunywa soda na kisoda.

Kikombe cha chupa ya chai ni kwa ajili ya kutoa msaada kwa mfuniko wa chupa ili ikiwa kuna hali ya baridi toka nje isije ikaingia kupitia mfuniko kirahisi na kile cha ndani kikapoa. Yaani kikombe kinaongeza usitiri wa kile kilichowejwa ndani ya chupa kisipoe kirahisi. Kitatumika tu pale ambapo imetokea dharura ya uhaba wa vikombe kama shambani, safarini, n.k

Sasa tuachane na hayo maelezo. Ni kitu gani nataka kukuambia muda huu?

Wengi tunatazama elimu, cheo, nafasi, uwezo, ujuzi, mali, n.k kama ndo njia za kufanikiwa kwenye maisha. Na tunachukua hivyo vitu kama ndo hatima yetu hapa duniani na pengine umemaliza yote na sasa “acha roho yako istarehe na kufurahi”. Kumbuka ya yule tajiri mpumbavu (Lk. 12:13-21).

Mpendwa, hayo ni ziada tu. Siku ya mwisho hutapimwa kwa elimu, fedha wala chochote unachokitumainia. Utapimwa kwa sheria ya upendo ambao ni amri kuu. Fedha, elimu, cheo, nafasi, uwezo, ujuzi, mali, n.k ni nyenzo tu za kujaribu kuonesha una upendo kiasi gani kwa Mungu na kwa watu wa Mungu, ingawa hata hivyo haviwezi kukamilisha tafsiri ya upendo pia.

Mungu anataka utumie hivyo vya nje kiimani ili vitunze kile cha thamani zaidi alichokupa ndani yako na kwenye maisha yako. Vya nje ni thamani za kidunia, ndani yako kuna mbegu ya Kimungu ambayo imebeba kusudi la wewe kuumbwa. Basi kuu zaidi ni lile la ndani ambalo linakuja kuvishwa kilemba na yale ya nje. Hii ina maana kuwa hata bila ya yale ya nje basi lile la ndani litadumu. Je, kichwa bila kilemba akili haziwezi kuwepo? Lakini kwenye baridi kilemba chaweza kusitiri kichwa; hata hivyo akili ya kutafuta kilemba ipo kichwani pia.

Inawezekana nimeongea kwa ugumu lakini mimi nazungumza kuthaminiana na kuishi kwa upendo wa kweli kwa Mungu na wanadamu. Usijione bora sana wala kujikweza maana utashushwa. Kumbuka kilichomuondoa shetani mbinguni ni dhambi ya Kiburi.

Mtu bora zaidi na anayemtumikia Mungu sawasawa ni yule ambaye maisha yake yameweka kitu chema kwenye mioyo ya watu kulingana na kile kile alichopewa na uwezo ule ule aliojaaliwa na Mungu. Ukifa umekufa wewe, lakini hakikisha kuna kitu kinabaki duniani na kwenye mioyo ya watu ili ijulikane uliishi duniani. Hakikisha husahauliki kama makapi shambani, tumia kikombe cha chupa ya chai kutunza joto na si kikombe cha chupa ya chai kunywea chai utapoteza joto la chupa yako.

Kikombe cha chupa ya chai ni elimu, cheo, nafasi, uwezo, ujuzi, mali, n.k na joto la ulichobeba ni lile kusudi la Mungu kwako. Kunywea kikombe cha chupa ya chai ni kule kutumia ulivyonavyo kuwakandamiza wengine na kuwa na kiburi.

Naitwa Mw. Benson Mmari, Shalom!

Ili kupata Makala zaidi na kwa njia rahisi, Install App yetu kwenye PlayStore. Tafuta BEWIS APA, au BONYEZA HAPA



TUAMBIE UNA MAONI GANI JUU YA HILI?

Facebook Plugin by princebewisa

Chapisha Maoni

Enenda kwa hekima, ukijua ni yapi yaliyo mapenzi ya Mungu huku ukiukomboa wakati. Install Bewisa App kwenye PlayStore kwa maarifa zaidi.
- EV. BENSON W. MMARI, +255 768 111 279

CodeNirvana
© Copyright Bewisa App | ™ - Efe. 5:15-17 | Modified By PB Web and Graphics
Back To Top