WAPENI NINYI CHAKULA |BY PRINCE BEWISA - Fahamu zaidi Staili za Maisha na Saikolojia. Bewisa App | ™ - Efe. 5:15-17
SOMA HIZI PIA:
Loading...

WAPENI NINYI CHAKULA



UNAWEZA KUPATA STORI ZETU MOJA KWA MOJA KWA KUBONYEZA 'LIKE' HAPA



« Piga 0652262137 kuweka tangazo lako hapa - Push kwa Buku tu »


Luka 9:10-17

Basi wale mitume waliporudi walimweleza mambo yote waliyoyatenda; akawachukua, akaenda nao faraghani mpaka mji mmoja uitwao Bethsaida. Na makutano walipojua walimfuata; akawakaribisha, akawa akisema nao habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa. Na jua likaanza kushuka; wakamwendea wale Thenashara, wakamwambia, Uage mkutano, ili waende katika vijiji na mashamba ya kandokando wapate mahali pa kulala na vyakula, maana hapa tulipo ni nyika tupu. Akawaambia, Wapeni ninyi chakula. Wakasema, Hatuna kitu zaidi ya mikate mitano na samaki wawili, tusipokwenda tukawanunulie watu hawa wote vyakula. Kwa kuwa wanaume waliokuwako walipata kama elfu tano. Akawaambia wanafunzi wake, Waketisheni watu kwa safu, kila safu watu hamsini. Wakafanya hivyo, wakawaketisha wote. Akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni akavibariki, akavimega, akawapa wanafunzi wake ili wawaandikie mkutano. Wakala, wakashiba wote; na katika vile vipande vilivyowabakia walikusanya vikapu kumi na viwili.

....................................

Somo hili lina kichwa kinachotutuma jambo fulani kwa watu fulani ambao wanatuzunguka. Ni agizo la Yesu Kristo kwa wanafunzi wake wakati ule alipokuwa akishirikiana nao kufanya huduma. 

Sisi wa leo tuliobatizwa na kuingizwa katika Pendo kuu la Mungu na Ufalme wake tumeitwa na kufanywa tayari kwa utume wa kila siku kwa kila ambaye yupo mbele yetu ili kutafsiri na kumwonesha sura na mfano wa Mungu kwenye yale ambayo tumejaaliwa kuwa nayo,  pasipo kujali kiasi na utoshelevu wake kwetu. 


Kupitia kisa hiki, Yesu anatutuma kuwapa wenye njaa chakula. Unaweza ukatazama hapo ukajiuliza, kwanini awaambie wanafunzi wake "wapeni ninyi chakula" ili hali alifahamu fika kuwa hawa wanafunzi hawakuwa na chakula pale? Hii inatupa somo:

1. Kabla hatujamwombea mtu kitu kwa Mungu tuhakikishe kuwa tumempenda sisi na kuwa tayari kumpa sehemu ya vilivyo vyetu ili kumsaidia kuvuka. 

2. Hata kama unajiona huna kitu, Mungu anaona kitu zaidi ndani yako kuliko ujionavyo wewe. Una uwezo wa kufanya mambo makubwa kuliko unavyojiona. Yesu aliona uwezo wa wanafunzi kulisha makutano ingawa wao hawakuona huo uwezo. Sawa na wewe ambaye na mahali unapitia, ama kuna jukumu zito limekufika, uwe na uhakika una uwezo wa kulikabili hata kama huoni uwezo huo ndami yako. Muamini Kristo tu nawe utafanya maajabu. 

3. Hatukupewa ili viwe vyetu tu bali tumepewa ili tuvitunze, tuvitumie na tuwatunze wengine na kisha tutoe hesabu. Wapo wanaokuzunguka, kabla hujaomba neno kwa Bwana basi hakikisha unawapa ulivyojaaliwa. Jilindeni na choyo na kila namna ya mambo kama hayo kwa watu na kwa Mungu ili kazi zake zidhihirike kwenye maisha yenu (soma Luka 12:15 na Wafilipi 2:3)

WAPENI NINYI CHAKULA

Ili kupata Makala zaidi na kwa njia rahisi, Install App yetu kwenye PlayStore. Tafuta BEWIS APA, au BONYEZA HAPA



TUAMBIE UNA MAONI GANI JUU YA HILI?

Facebook Plugin by princebewisa

Chapisha Maoni

Enenda kwa hekima, ukijua ni yapi yaliyo mapenzi ya Mungu huku ukiukomboa wakati. Install Bewisa App kwenye PlayStore kwa maarifa zaidi.
- EV. BENSON W. MMARI, +255 768 111 279

CodeNirvana
© Copyright Bewisa App | ™ - Efe. 5:15-17 | Modified By PB Web and Graphics
Back To Top