SEMINA WA WABABA (WANAUME) |BY PRINCE BEWISA - Fahamu zaidi Staili za Maisha na Saikolojia. Bewisa App | ™ - Efe. 5:15-17
SOMA HIZI PIA:
Loading...

SEMINA WA WABABA (WANAUME)



UNAWEZA KUPATA STORI ZETU MOJA KWA MOJA KWA KUBONYEZA 'LIKE' HAPA



« Piga 0652262137 kuweka tangazo lako hapa - Push kwa Buku tu »

 

Picha: Mtazamo ya maisha ni kama safari ndefu na wakati mwingi kuna njia panda kadhaa. 

NAFASI YA MWANAUME 

Siku yoyote, mahali popote ukisikia kimepigwa kigelegele kwamba amezaliwa mwanaume, basi, ujue hicho kilichozaliwa ni kiumbe kinachoeleweka. 


Somo: Mwa. 3:8-9 "Adamu uko wapi?"

- Mungu anajua yote, anaona yote, lakini kwanini aliuliza uko wapi na kwanini swali hili hakumuuliza Eva licha ya kuwa Eva ndiye aliyekula tunda? Kwanini Adam? Una kitu kwa mwanaume.

- Ni lazima Mungu ahusike kwenye maisha yako. Jasho pekee halitoshi, unamhitaji Mungu ajihusishe; ili ajihusishe anatokea kwenye nafasi yako. Kwa hiyo lazima ukae katika nafasi yako.

- Kwa hiyo, Mungu anapomuuliza Adamu uko wapi maana yake alimtazama kwenye nafasi (is the matter of position) - Zab. 31:2b

- Mambo yaliyopo kwenye nafasi:

    * Uwajibikaji 

    * Nafasi yoyote ina fursa

    * Nafasi yoyote ina makusudi ya Mungu

Kama ni hivyo, lazima mwanaume uwe sahihi kwa 100% kwenye nafasi yako kwa sababu wewe ni kichwa. Kichwa maana yake ni umiliki, utawala, kuongoza, kuwajibika, n.k

Lazima iwe 100% kwa sababu kwenye maisha kuna vitu vinahitaji "precision" usahihi katika uwajibikaji. Kwa hiyo mwanaune ukiyumba kidogo, kuna kitu kitaharibika. 

Jaribu kufikiria kiongozi wa ndege huko Frankfurt alikuwa akifanya vema kwa 99% kwenye kazi yake. Maana yake ni kuwa, 1% ilipotea katika uwajibbikaji wake. Kwa hiyo, hii ni kusema, kwa kila ndege 100 alizoongoza, basi ndege moja ilipata shida kiuongozaji. 

Mwanaume huyu, kibinadamu hawezi kuwa sahihi 100% badala yake ili iwe hivyo anamhitaji Mungu sana na neema zake. Kwa sababu "si kazi ya mikono iletayo wokovu, bali neema".

Mwanaume lazima uwe kiongozi. Kiwa kiongozi maana yake ni "Artitecture" (mchoraji) yaani aone mambo kabla hayajatokea. Kwa hiyo, ili maono hayo yawepo, unahitaji kuwa timamu na mwenye kukaa kwenye nafasi mbele za Mungu. 

Baba ni mbeba maono (msanifu) na mama ni mtendaji (injinia mjenzi). Ukikuta familia inaongozwa na mwanamke hiyo ni ajali. Ni kama treni ambayo kichwa kipo nyuma mkia upo mbele. 

Mwanamke akiongoza familia na mwanaume upo, uwe na uhakika kuna mahali anakwendaga kupata ushauri. Lazima ukae kwenye nafasi yako na ujue unahitaji msaada wa Mungu. Ifike mahali tuone ni kinababa ndo wanaogaragara madhabahuni kutafuta msaada wa Mungu. 

^Mch. Wilbroad Mastai


..........................................................


JUKUMU/MAMLAKA YA BABA

(Malaki 4:4-5; Yn. 7:38)

- Kiongozi mzuri ni yule ambaye anasoma kanuni na kujua maelekezo juu ya nafasi yake. Mwanaume ni kiumbe kinachotakiwa kuongoza sawasawa na makusudi ya Mungu, kwa hiyo mwanaume hakuna mahali popote tunaweza kumuona Mungu akitoa maelekezo isupokuwa kwenye Neno lake. Akili ya Kristo ipo kwenye Neno na hakuna kitakachotokea kwetusawa na mapenzi yake isipokuwa kimetokana na Neno lake (Yn. 1:1ff)

- Mwanaume ni lango la baraka; na hili ili liwezekane, lazima asimame kinyume na laana zozote. Laana ni kitu chochote ambacho kipo kinyume na baraka. 

- Mwanaume akijaa Neno la Mungu na kwakuwa amejaa mamlaka makubwa, basi atakuwa chanzo cha maji yaliyo hai. Neno la kinywa chako litajaa uhai na baraka kama Neno la Kristo kwa yule mwanamke Msamaria. Mwanaume kama kichwa cha familia lazima awe chemchem iliyo hai. 

- Katika Mwanzo 49:9 tunaona habari za Yakobo ambapo mstari wa uchumi (economy graph) kutokea nyumbani ulikuwa juu, lakini uzao wake unahaha kuwa na mwendelezo huo wa kiuchumi. Fikiria mpaka wanahama Israel kwenda Misri kwa ajili ya njaa, maana yake grafu ya uchumi ilishuka mpaka chini kabisa kwenye mstari wa hasi, ni mpaka Yusuph alipokuja na kuweka sawa baadae. Kwanini hivi? Yakobo alijaa uchungu kwa watoto wake na hakupata mahali mahali pa kuhemea. 

Sasa familia nyingi na wanaume wengi Afrika tupo kwenye hali hiyo, kwamba wanapambana sana kufanikiwa lakini hawarithishi tabia ya mafanikio na baraka kwa watoto wake; kwanini, ni kwa sababu ya uchungu kwa watoto na kushindwa kutumia fursa ya Neno la Mungu kusafisha nafsi na mwisho unakuta analia ndani kwa ndani na akitamka kitu kwa mtoto ni laana (pitia Mwa. 49).

Kama Yakobo angeongea mapema watoto wake wasingefika hapo. Wanaume tutumie majukwaa yetu kuongea, tusema mambo mapema na tutumie Neno kufuta uchungu. Tuwe chanzo cha mito ya maji yaliyo hai na si laana kwa watoto. Turithishe watoto miji mizuri, mali, uwezo wetu, n.k

- Tusimame kwenye nafasi zetu tumlingane Bwana, tujenge misuli ya kiimani na tuwe chimbuko la baraka kwa Mungu. 

^Mch. Anta Muro 

Ili kupata Makala zaidi na kwa njia rahisi, Install App yetu kwenye PlayStore. Tafuta BEWIS APA, au BONYEZA HAPA



TUAMBIE UNA MAONI GANI JUU YA HILI?

Facebook Plugin by princebewisa

Chapisha Maoni

Enenda kwa hekima, ukijua ni yapi yaliyo mapenzi ya Mungu huku ukiukomboa wakati. Install Bewisa App kwenye PlayStore kwa maarifa zaidi.
- EV. BENSON W. MMARI, +255 768 111 279

CodeNirvana
© Copyright Bewisa App | ™ - Efe. 5:15-17 | Modified By PB Web and Graphics
Back To Top