RATIBA YA JUMA TAKATIFU NA MAMBO MUHIMU KUFAHAMU KWA KIFUPI |BY PRINCE BEWISA - Fahamu zaidi Staili za Maisha na Saikolojia. Bewisa App | ™ - Efe. 5:15-17
SOMA HIZI PIA:
Loading...

RATIBA YA JUMA TAKATIFU NA MAMBO MUHIMU KUFAHAMU KWA KIFUPI



UNAWEZA KUPATA STORI ZETU MOJA KWA MOJA KWA KUBONYEZA 'LIKE' HAPA



« Piga 0652262137 kuweka tangazo lako hapa - Push kwa Buku tu »


KWA AMBAO HAWAJUI RATIBA YA WIKI HII KUU YA MATESO YA BWANA WETU YESU KRISTO KATIKA LITRUJIA YA KANISA, IKO KAMA IFUATAVYO:-

1. JUMATATU KUU

Hii ni siku maalumu ambayo Yuda anajitoa mwenyewe kabisa katika Jumuiya ya Mitume, na kuanza mipango yake kabambe ya kumuuza Yesu.

2. JUMANNE KUU

Hii ndiyo siku ambayo Yuda anatimiza mipango yake ya kumsaliti Yesu na kukabidhiwa vipande thelathini (30) vya fedha.

3. JUMATANO KUU

Hii ndiyo siku ambayo Yesu anawajulisha na kuwatangazia Mitume wake juu ya mpango wa Yuda, japo kwa mafumbo na kueleza waziwazi yale yatakayompata.

4. ALHAMISI KUU

Hii ndiyo siku ambayo, wakati wa jioni Yesu anaweka sakramenti kuu mbili ambazo ni: EKARISTI TAKATIFU na DARAJA TAKATIFU pamoja na AMRI KUU YA MAPENDO.

5. IJUMAA KUU

Hii ndiyo siku ambayo, asubuhi na mapema (Alfajiri) Yuda anapokea kikosi cha maaskari tayari kwa kumsaliti Bwana wake, Mwalimu na Muumba wake.

Hapa naomba niseme kidogo, kwa utamaduni wa Waisraeli kulikuwa na salamu za mabusu za aina tatu (3) ambazo ni:

1. Salamu ya Bwana na Mtumwa - ambapo mtumwa alitakiwa kulala kifudifudi na kubusu miguu ya Bwana wake.

2. Salamu ya Mwalimu na Mwanafunzi wake - ambapo mwanafuzi alipaswa kupiga goti moja na kubusu mkono au mikono ya Mwalimu wake. Na hii ndiyo salamu ambayo Yuda alipaswa kumsalimia Bwana Yesu siku zote hata pale bustanini Gethsemane. Kwani hata Watumishi wa Altare hufanya hivi pale wanapokutana na Mapadre au wakati wa kutoa amani.

3. Salamu ya Mwalimu kwa Mwalimu, Bwana kwa Bwana, Wakuu kwa Wakuu -  Mara nyingi hawa husalimiana kwa kubusiana mashavu wakiwa wamesimama.

Mpaka hapo mtakuwa mmelewa jinsi usaliti wa Yuda ulivyokuwa mkubwa, na nini maana ya swali la Yesu kwa Yuda aliposema: " Yuda unamsaliti Mwana wa Adamu kwa kumbusu?

Pia siku hiyo hiyo ya IJUMAA KUU, Yesu anahukumiwa afe majira ya saa 3:00 asubuhi, saa 6:00 mchana anasulubiwa, saa 9:00 alasiri anakufa pale Msalabani na saa 12:00 jioni anazikwa ili kupisha Sabato iingie.

6. JUMAMOSI KUU

Hii ni siku ambayo kwa lugha nyingine huitwa BLACK SATURDAY (Jumamosi Nyeusi) kwa sababu Bwana wa Sabato yaani Bwana wa Kanisa yuko kaburini.

Wanateolojia wanasema: Yesu alikwenda kuzimu kumnyang'anya ufunguo shetani wa kuimiliki dunia na kuzihubiria roho zilizoko kule ambazo hazijawahi kusikia Mafundisho ya Neno la Mungu na kwenda nazo Mbinguni.

Na wakati huo huo pia alikwenda Toharani na Limbo, ili kuzitia moyo roho za Watakatifu zilizoko kule, zinazosubiria sala zetu na Huruma ya Mungu ili nazo ziende Mbinguni.

Hivyo katika siku hii Kanisa linakuwa kimya, na wala hakuna Ibada yoyote itakayofanyika siku hiyo, kwa kuwa Yesu yuko kaburini. Lakini pia usiku huo wa BLACK SATURDAY,  ndiyo siku tunayoanza Vijilia au Mwanzo la Kesha la Yesu Mfufuka.

7. JUMAPILI KUU

Hii ni siku ambayo, Yesu Mfufuka anafufuka kutoka kaburini na kushinda mauti. Na katika siku hii, ndiyo siku iliyowekwa misingi mipya ya Kanisa, yaani kutoka kuabudu siku ya Jumamosi na kuanza Kuabudu siku ya Jumapili.

Nakutakia tafakari njema pamoja na toba ya kweli. Bwana asikie kuomba kwako. 

Ili kupata Makala zaidi na kwa njia rahisi, Install App yetu kwenye PlayStore. Tafuta BEWIS APA, au BONYEZA HAPA



TUAMBIE UNA MAONI GANI JUU YA HILI?

Facebook Plugin by princebewisa

Chapisha Maoni

Enenda kwa hekima, ukijua ni yapi yaliyo mapenzi ya Mungu huku ukiukomboa wakati. Install Bewisa App kwenye PlayStore kwa maarifa zaidi.
- EV. BENSON W. MMARI, +255 768 111 279

CodeNirvana
© Copyright Bewisa App | ™ - Efe. 5:15-17 | Modified By PB Web and Graphics
Back To Top